06/07/2022
🇨🇩💪🏿💪🏿🇷🇼
Kurejea kwa ukawaida wa diplomasia kati ya DRC na Rwanda, M23 kuondoka bila masharti popote pale wanapomiliki kwenye ardhi ya DRCongo, hayo yakiwa ni baadhi ya maamuzi muhimu yaliyofikiwa na viongozi walioendesha mazungumuzo ya kuwakutanisha Felix Tshisekedi wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda, kutafuta suluhu kwenye mzozo unaoshuhudiwa kati ya DRC na Rwanda, mjini Luanda nchini Angola, leo Jumatano Julai 06, 2022.