New Safari Ya Mahusiano/Ndoa

New Safari Ya Mahusiano/Ndoa Mahusiano Ni Maisha, na maisha bila mahusiano bora hayawezi kuwa bora
Karibuni katika safari ya Mahusiano...

Mapenzi ni Nini??
27/12/2025

Mapenzi ni Nini??

Maisha ya mapenzi ni uamuzi, hakuna kosa kumpenda mtu. Mbaya ni kumpata limbukeni wa mapenzi akauchokonoa ubongo wako, h...
20/12/2025

Maisha ya mapenzi ni uamuzi, hakuna kosa kumpenda mtu.
Mbaya ni kumpata limbukeni wa mapenzi akauchokonoa ubongo wako, heshima yako na mwili wako.

MUHIMU KWA WANAUMESaikolojia ya MwanamkeMaelezo haya yanatoa mafunzo kuhusu tabia na akili ya mwanamke wakati anapoingia...
08/10/2024

MUHIMU KWA WANAUME

Saikolojia ya Mwanamke
Maelezo haya yanatoa mafunzo kuhusu tabia na akili ya mwanamke wakati anapoingia katika mapenzi na mwanaume. Na hasa mwanamke anapokuwa mrembo, fahamu atakujaribu bila hata ya yeye mwenyewe kujifahamu. Ukiweza kufaulu kwenye majaribu hayo, she feels like wow na anaanza kupenda na kukupa heshima. Lakini ukishindwa kukabiliana na majaribio hayo kinachotokea ni kwamba wewe mwanaume unakua chini yake na yeye mwanamke anakuwa juu. Na hayo ndio matakwa ya mwanamke kwa uhalisia.

Saikolojia 01 : Upendo na Uhitaji
Mwanamke huwa na kawaida ya kuangalia uhitaji wa mwanaume. Anapenda kufahamu ni kwa kiasi gani mwanaume huyu ananipenda na kwa kiasi gani ananihitaji kiasi ya kuwa anashindwa kunikosa. Anapofahamu ya kuwa wewe unahitaji sana kutoka kwake, huanza kutumia udhaifu huo kukamilisha matakwa yake binafsi k**a vile kufanya vitu kwa uhuru n.k. Hivyo huanza kuchukua mamlaka tataribu na kujaribu kukudhibiti kupitia huo upendo unao-muonesha. Ili kufaulu hapa unatakiwa kuonesha ya kwamba unamjali lakini na unampenda lakini ujaribu kumfanya akubali ya kuwa sio muhitaji sana kwake. Kwa mfano k**a umetaka kitu kutoka kwake na yeye amekunyima usioneshe kuwa ulikuwa unahitaji sana. Nyamaza kimya na wala usirudie kumuomba kila wakati kitu hicho. Ukifanya hivyo, mwanamke hufikria wewe hauna thamani. Lakini unapo onesha ya kwamba huna haja naye sana, kile ulichokitaka utapewa kwa upendo zaidi kuliko k**a ungeliendelea kusisitiza. Ukitaka kitu kutoka mwanamke jifanye k**a huna haja nacho, atakupa zaidi ya ulivyotaka.

Saikolojia 02: Kusoma mazingira.
Mwanamke huwa na kawaida ya kukusoma tabia zako wewe mwanaume pale munapokuwa katika mahusiano. Wakati unahitaji mapenzi na kutimiza hisia zako, yeye huangalia kwenye tabia zako, jinsi ulivyo, mkarimu, mkatili, mwenye hasira, mpole n.k Yote hayo humsaidia kukufahamu wewe na kuanza kutumia sehemu yenye udhaifu k**a ushindi kwake. Hii ni kwasababu mwanamke anapenda sana uhuru wake lakini wakati huo huo anahitaji upendo pia. Kwa mfano, siku za mwanzo mwanzo kwenye ndoa na mahusiano anaweza kutoka bila ya kupata ruhusa, anakuangalia jee utafanyaje? Utakemea au utanyamaza kimya au utachukulia ni jambo la kawaida tu. Hapo huangalia jinsi utavopokea, anapofahamu ya kuwa kitu fulani hakijakukera na wala hukuonesha hisia yoyote katika jambo anaendelea kufanya kitu hicho kwa mara nyingine mpaka anathibitisha ya kuwa hujali kwenye hilo. Sasa siku ambayo utahitaji kumzuia, ndipo hapo ugomvi unaanza. Ili kufaulu hapa, k**a kitu chochote hujapenda kutoka kwake ni bora uwe muwazi tokea mwanzo. Watu wengi huharibu hapa, kwasababu mwanamke unampenda sana na labda unahisi k**a utaongea chochote anaweza kukuacha unaamua kukaa kimya, fahamu ya kuwa unampa uhuru amabo utakuharimu baadae. Unaposema kitu fulani hukipendi tokea mwanzo mwanamke anatengeza heshima anajua ya kuwa unampenda lakini wakati huo huo unamfanya afahamu ya kuwa maisha yako yana thamani zaidi kuliko mahusiano.

SAIKOLOJIA 03: Vice Versa
Hii ni tabia nyengine ya mwanamke, anaposema kitu fulani atafanya aidha kwa kumuomba au kwa kutaka mwenye, fahamu kuwa kwa 90% hatofanya kitu hicho. Usitie tamaa kabisa k**a atafanya, chukulia k**a vile hajawahi kukuahidi chochote. Na anaposema kitu fulani hatofanya basi kwa 75% atafanya kitu hicho. Hivyo zikitokezea hali k**a hizi usikurupuke wewe mchukulie k**a alivyo. Hii ni kwasabau akili ya mwanamke inapoingia kwenye huwa k**a mtoto.

SAIKOLOJIA 04: Kudeka au Kujibebisha
Mwanamke hupenda sana kudeka au wanaita kujibebisha, hii ndio asili ya mwanamke na k**a utamuona mwanamke hana tabia hiyo aidha ameshaumizwa sana au amerithi tabia za kiume. Hivyo anapojibebisha unatakiwa kuenda nae vizuri. Wanaume wengi pia huharibu hapa, wanapomuona mwanamke anajidekeza wao hukemea tabia hiyo. Kitendo hiki kwa 60% kinapunguza mapenzi kutoka kwake mwanamke. Kauli k**a “hemu, niache nipo busy” utazisikia kutoka kwa mwanaume.

SAIKOLOJIA 05: Maamuzi
Hii ni sehemu muhimu sana ambayo mwanaume unatakiwa kufaulu. Mwanamke huwa na kawaida ya kuangalia uamuzi wako. Kwa mfano, tuchukulie mkeo anakwambia baba fulani leo nahitaji ubakie nyumbani usiende kazini. Huenda hapo hakusema hivyo kwasababu ana hamu na wewe, pengine alikuwa anaangalia utachukua uamuzi gani? Ukikubali haraka na mara moja itakuwa umempa thamani na hiyo itamfanya yeye kupoteza mvuto kwako, Ukikataa moja kwa moja unatengeneza picha ya kutomjali. Sasa unafanyaje? Unatakiwa usikubali lakini utafute sababu au sharti. Kwa mfano, unaweza kusema hivi, sawa ukitaka nibakie basi nipige busu au nikumbatie. Mwanaume wa design hizi anavutia sana kwa mwanamke yoyote yule.

SAIKOLOJIA 06: Kuepuka au Kupunguza upendo
Mwanamke pia anakuwa na tabia ya kukuepuka au kuonesha hakupendi tena au kuonesha upendo wake umepungua, na hii inatokea baada ya kuishi nae kwa muda mrefu. Ingawa kwa uhalisia anakuwa anakupenda tena sana lakini hufanya hivyo ili kujua udhaifu wako. Kuangalia jee kwa kutumia silaha hiyo anaweza kukuburuza. Kwasababu matakwa makubwa ya mwanamke ni kumuendesha mwanaume vile anavyotaka yeye. Sasa ili kufaulu jaribio hili, usikurupuke isipokuwa muoneshe wewe upo sawa na hali yoyote hile hata k**a kumkosa ikibidi. Wapo wanaume wengine katika hali k**a hiyo, huanza kuzalisha mashaka kwenye uhusiano na kummuliza mwanamke unanipenda au kwanini umepungua upendo wako. Unapofanya hivyo tu, kaka unafeli.

SAIKOLOJIA 07: Hofu ya kuachwa.
Mwanamke anapojihakikishia ya kuwa anampenda mtu fulani inakuwa ni kweli kabisa tofauti na mwanaume. Ndio maana mwanamke hawezi kugawa penzi lake, hata k**a atakuwa na wanaume 2 au zaidi ya hapo, kuna mmoja anampenda kweli na wengine waliobakia anawadanganya. Sasa, mwanamke huogopa sana kuachwa na mtu anaempenda kwa dhati, jambo hilo humtia hofu sana. Hivyo epuka tabia za kutania kuwa unataka kumuacha mwenza wako. Kwani kufanya hivyo, hupelekea kupunguza mapenzi ya mwanamke na kumfanya ajenge chuki taratibu dhidi yako.

SAIKOLOJIA 08 : Kuweka Refrence
Sijapata kuona sehemu ambayo wanawake wapo vyema k**a hapa. Wapo vizuri sana kwenye kuhifadhi mambo. Wewe unaweza kupandisha hasira na kuongea mbovu vya kutosha halafu baada ya muda ukasahau na ukasamehe pia. Lakini mwanamke chochote utachokisema yeye hunakili na kukiweka akilini. Na sio hapo tu, bali hutengeneza tafsiri. Hivyo ni jambo zuri k**a ukipandisha hasira kubakia kimya na kutoa maamuzi baadae. Lakini pia unapoweka ahadi kwa mwanamke jikubalishe ya kuwa utatimiza ahadi yako. kwasababu hata iweje ujue mwanamke kitu hicho atakuwa na kumbukumbu nacho. Ni bora usi-ahidi k**a huwezi kutekeleza, kwanini? Kwasababu kwa kitu kidogo k**a hiko tu, kwa mwanamke kumtia uchungu sana mpaka pale utakapotimiza.

SAIKOLOJIA 09: Hakubali kushindwa
Wanawake wana kitu kinaitwa “Complex Superiority Psychology”. Kisaikolojia hali hii inamfanya mtu kujiona yeye yupo sahihi zaidi au anaweza kufanya kitu kwa ufanisi zaidi kuliko mwengine. Hivyo kwa mwanamke ni bora afe lakini anapoamua kusimamisha misimamo yake huonesha yupo bora sana.

USHAURI WA BURE KWA WAZAZI:MAMBO ANAYOTAKIWA KUZINGATIA MZAZI YA KUFANYA MTOTO AKIWA LIKIZO:Kipindi hiki watoto wetu wam...
11/12/2022

USHAURI WA BURE KWA WAZAZI:
MAMBO ANAYOTAKIWA KUZINGATIA MZAZI YA KUFANYA MTOTO AKIWA LIKIZO:
Kipindi hiki watoto wetu wamerudi kwa ajili ya Likizo ni vizuri wazazi kuzingatia haya:
1. Jipe muda wa kuzungumza na MTOTO Kila Siku.
2. Muulizie juu ya Changamoto alizokutana nazo akiwa shule.
3. Kagua vitu anavyovitizama km picha, simu.
4. Jadiliana naye kuhusu matokeo yake ya mwaka mzima.
5. Kuwa makini sana na aina ya marafiki anaokuwa nao ikiwezekana angalia background ya familia za marafiki wake.
6. Mpe muda wa kwenda kwa wazazi wa pande mbili ajifunze mahusiano na familia.
7. Hakikisha anapata muda wa kiroho kushiriki ibada na pia muombe pamoja.
8. Usimpe Kila anachotaka Mpe kwa sababu ni muhimu.
9. Usimdekeze afanye kazi za mikono hata K**a una dada au kaka kazi aoshe vyombo, asafishe Nyumba, atandike chumba chake, afue nguo mwenyewe na hata kuhudumia kazi za uzalishaji hapo nyumbani.
10. Epukeni magomvi ya Mara kwa Mara yatakayomfanya aathirike kisaikologia.
11. K**a mmeachana na mzazi mwenzako Hakikisha MTOTO anapata nafasi ya kumsalimia mzazi mwenzako.
12. Usiruhusu MTOTO kushinda peke yake chumbani akicheza game Mpe nafasi ya ku-sociliaze lakini kuwe na mipaka
13. K**a Kuna kazi za kijamii k**a kutembelea yatima Mpe muda afanye charity work itampa tabià ya kujali wwngi.
14. Epuka Sana kuonyesha kuwa una muogopa na analosema utatekeleza mahali Fulani lazima kuwa strictly.
15. Mpangie revision kwa kiwango Ili akili ipumzike.
16. Anza kujadiliana naye kipawa chake na ndoto zako.
17. Mueleze Changamoto zilizopo km UKIMWI, USHOGA na tabià hatarishi.
18. Mfundishe unyenyekevu na kuheshimu wengine
19. Mtie moyo ukimjengea uwezo wa kuwa Anaweza
20. Jadiliana naye Hali ya uchumi ilivyo katika familia ajue katika maisha Kuna up and down na mfundishe Umuhimu wa ku-share Changamoto alizonazo.Niwatakie kazi njema na Malezi Mema kwa Watoto wetu na Mungu atubariki sana.🙏🙏

Dear My BrotherSIKU ZOTE UNAWEZA KUMTONGOZA MWANAMKE AKAKUKUBALIA HAPO HAPO, ILA ILI AKUPENDE UNATAKIWA KUFANYA KAZI YA ...
03/07/2022

Dear My Brother

SIKU ZOTE UNAWEZA KUMTONGOZA MWANAMKE AKAKUKUBALIA HAPO HAPO, ILA ILI AKUPENDE UNATAKIWA KUFANYA KAZI YA ZIADA, MAANA WENGI WAO BADO WANA MAKOVU YA USALITI NA WOGA WA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO✍🏽✍🏽

Share...

Simamia NDOA yako na ilinde na maadui toka nje. Acha Familia yako, ndugu na marafiki zako wafahamu kuwa linapokuja suala...
05/04/2022

Simamia NDOA yako na ilinde na maadui toka nje. Acha Familia yako, ndugu na marafiki zako wafahamu kuwa linapokuja suala la NDOA yako kuna mstari wanapaswa wasivuke. K**a ni kuchagua upande, basi chagua upande wa NDOA yako.

Tokea ile siku ulivyotamka mbele ya madhabahu kwamba 'Ndio nakubali' basi, mwenza wako ndipo alipokua kipaumbele chako cha kwanza. Simama na mpenzi wako, mtetee kwa kila hatua anayopitia, na k**a anasakamwa na ndugu zako, basi ndio muda sahihi wa kumaanisha kile kiapo ulichoapa mbele za MUNGU kwamba utakuwa nae katika dhiki na faraja.

Usimwache ahangaike na kuumia peke yake! Wewe ndio faraja yake na mlinzi wa karibu!! "Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu (Baba, mama, kaka, dada, shangazi, wajomba, marafiki, bibi) asikitenganishe.💯👨‍❤️‍💋‍👨💦

Senegal 0-0 Misri (P..4-2)Senegal wanaweka rekodi kwa kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza.
06/02/2022

Senegal 0-0 Misri (P..4-2)

Senegal wanaweka rekodi kwa kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza.

Gusa link tujumuike Group la Mahusiano whatsappKaribuni sana Kwa watu wenye nidhamu na kujitambua
21/01/2022

Gusa link tujumuike Group la Mahusiano whatsapp

Karibuni sana
Kwa watu wenye nidhamu na kujitambua

WhatsApp Group Invite

Ulimi Wako Usiutumie Kutaja Aibu ya Mtu, Kwani hata wewe Umejaa Aibu, Na Watu Pia wanazo Ndimi za Kusema Aibu zako, Pia ...
20/01/2022

Ulimi Wako Usiutumie Kutaja Aibu ya Mtu, Kwani hata wewe Umejaa Aibu, Na Watu Pia wanazo Ndimi za Kusema Aibu zako, Pia macho yako yakikuonyesha Aibu za Mtu, Basi liambie Jicho lako Kwamba, Ewe jicho, Watu Pia wana Macho, ya kuona aibu zangu Tujitahidi sana kurekebisha ya kwetu kabla ya kuhangaika Kutafuta ya Watu✍🏽✍🏽✍🏽

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255629064944

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when New Safari Ya Mahusiano/Ndoa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to New Safari Ya Mahusiano/Ndoa:

Share