Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid El Fitr inatarajiwa kuwa Machi 31 au Aprili Mosi kutegemea na mwandamo wa mwezi na kwamba kitaifa sherehe hizo zitafanyika jijini Dar es salaam.
#njoomoroupdates
Watu wawili wamejeruhiwa leo Jijini Dar es salaam baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari matatu katika katika maeneo ya daraja la Tanzanite baada ya Dereva Suleiman Firoza Jusa wa gari aina ya Toyota Crown kuwa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi.
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea baada ya Dereva wa gari namba T 641 DRC aina ya Toyota Crown akitokea Masaki kuelekea Upanga kugonga kingo kulikosababisha kuhama upande aliokuwepo na kuhamia upande wa pili wa barabara kwenye njia ya magari yanayotoka Mjini na kuyagonga magari mawili ambayo ni Toyota Hiace namba T 840 EDU likiendeshwa na Geofrey Bundala huku Volkswagen namba
T886EDA likiendeshwa na Markina Anderson.
Mmoja wa Mashuhuda wa ajali hiyo Said Matola Ali ameongea na AyoTV na kusimulia tukio hilo huku pia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo ni mwendo kasi wa Dereva wa Crown na kutojali kwake.
Tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 7.7 limeikumba Myanmar siku ya ljumaa, huku mitetemeko mikali ikiitikisa nchi jirani ya Kusini-mashariki mwa Asia ya Thailand.
Tetemeko hilo lilitokea katika kina cha kilomita 10, takriban kilomita 17.2 kutoka mji wa Mandalay nchini Myanmar, ambao una wakazi milioni 1.2, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS).
Jengo la ghorofa ya juu lililokuwa likijengwa liliporomoka kutokana na tetemeko la ardhi katika mji mkuu wa Thailand wa Bangkok, na kuua mtu mmoja, polisi wa eneo hilo walisema, na kuongeza kuwa wafanyakazi kadhaa waliokolewa.
Dakika chache baada ya kutoka katika Kikao cha pamoja na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Pro. Palamagamba Kabudi, Rais wa Yanga SC amesema wamefikisha ujumbe wao kwa Waziri huyo.
Waziri Kabudi amewaita viongozi wa timu za Yanga SC, Simba SC, TFF na TPLB kwa ajili ya kujadili suala la Mchezo wa Derby kushindwa kufanyika Machi 8 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Hersi alisema “Tumefikisha ujumbe wetu tuliokuwa nao kwa Waziri na niwahakikishie wanachama wa Yanga SC viongozi wao ni imara na tunapigania maslahi ya klabu yetu” alisema Hersi.
DAR ES SALAAM; Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya kupokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2023-2024 pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe MUSSA KILAKALA ametoa vyakula vya futar na Iddy kwenye Gereza la Wanawake Kingolwira na Gereza la Mahabusu Morogoro Pia Mkuu wa Gereza Wanawake Kingolwira SP. Atupelye luwanja amemshukuru mkuu wa Wilaya kwa moyo mzuri wakuwakumbuka wafungwa pamoja na SSP. ALFRED LEMGOHA MKUU WA GEREZA LA MAHABUSU MOROGORO amefurahishwa na kitendo hicho.
@mussa.kilakala
#njoomoroupdates #morogoro #tanzania
Mechi ya kirafiki iliyoandaliwa jana na lkulu ya Burkina Faso ilimshuhudia Nahodha Ibrahim Traoré aking’ara kwa kufunga mabao matatu (hat-trick), katika tukio la nadra analoonekana hadharani bila combat wala bastola kiunoni.
Tukio hili la ishara ya kuwa kiongozi huyo kijana kuliko wote anapenda michezo, lilipewa uzito zaidi na uwepo wa wachezaji nyota wa zamani wa soka barani Afrika, waliokuja kuonyesha mshikamano wao wa dhati kwa wananchi wa Burkina Faso.
#njoomoroupdates #ibrahimtraoré #burkinafaso
Katibu mwenezi wa Baraza la Wanawake la
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Taifa Sigrada Mligo ameonekana kwenye video hii akilalamika maumivu kwa kile kinachodaiwa kupigwa na vijana wa
hamasa wa chama hicho mkoani Njombe.
Tukio hilo linadaiwa kutokea wakati kikao cha ndani kilichokuwa kinaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa
CHADEMA John Heche kikiendelea.
Sasa pesa umepeleka wapi wewe dalali ...Jamani
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumanne Machi 25, 2025 Ofisini kwake Jijini Arusha, amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa, ambaye amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa tayari serikali imeanza taratibu za Ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ya kuunganisha mikoa ya Kaskazini
Kadogosa amemueleza Mhe. Makonda kuwa ujenzi huo unaofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ni maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ambapo sasa serikali ya awamu ya sita itajenga reli hiyo ya kisasa sambamba na kufanya maboresho kwenye reli ya Kaskazini, suala ambalo linatajwa kusisimua uchumi wa Arusha ambapo serikali pia ina mpango wa kujenga bandari kavu kwaajili ya kuhudumia shehena za mizigo zinazotoka bandari ya Tanga.
“Arusha ina maana kubwa sana, sio tu tunajenga reli ya SGR kuja huku lakini tuna sababu za kiuchumi, kuna madini soda pia ambayo ni uchumi mkubwa sana na yale machimbo yanaweza kuwepo zaidi ya miaka mia moja, lakini jambo jingine muhimu kwa watanzania ni ujio wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuja Tanga hii ina maana kuwa yale mafuta ili yaende kwenye nchi nyingine kuna namna mbili, ujenge bomba la mafuta safi ama utumie reli, kwahiyo reli hii ni muhimu sana kiuchumi. Amesema Kadogosa.
Kwa upande wake Mhe. Makonda amemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa maono yake kwa Mkoa wa Arusha, akiahidi kuwa Arusha itaweka rekodi kwa kura nyingi zaidi kwa Rais Samia Mwezi Oktoba mwaka huu, kama shukrani kwa miradi na fursa nyingi za maendeleo zilizotekelezwa ndani ya miaka minne ya uongozi wake ikiwemo ukuzaji wa uchumi na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara pamoja na uimarishaji wa sekta ya utalii na madini ambapo sasa Mkoa pia kwa kushirikiana na Wizara ya madini wameanza mpango wa kuwa na maonesho ya madini yatakayofanyika kwa mwaka mara moja mkoani hapa.
#tanzania #africa #arusha #kilimanjaro #sgr #njoomoroupdates
@hpolepole Kwa Waisalamu Asalaam Aleikhum Warahmatulahi taala Wabarakatu, kumbukeni kati ya nguzo tano za Uislamu ni pamoja na funga, msiache kufunga.
Kwa Wakristo Nawasalimu katika Jina la Bwana Wetu Yesu Kristo Mwana wa Mungu Aliye Hai, kumbukeni maelekezo ya kufunga yako katika maandiko ikiwemo Mathayo 6:16-18 na kwa faida yako malizia ule Mstari wa 19 hadi 21. Mbarikiwe mpaka mshangae!