03/10/2023
πππ πππππ ππππππππππ πππππππππ πππππππ.
Ukikaa kwenye Banda umiza utasikia mdundo wa Ngoma Wenye chuki na ukakasi kwa Simba Sc......Ukikaa kwenye vijiwe vya kahawa utasikia mlio wa Ngoma ukivuma Wenye kuleta Taharuki na mfarakano kwenye Benchi la Simba Sc...... Ukiwa kwenye Daladala utasikia mlio wa Ngoma ukikuhitaji uucheze hata K**a huelewi unataka uucheze vipi.
Lakini kwasababu Tumeamua kuucheza bila kuakisi mlio wa wapigaji, Basi tunajikuta tunaucheza tu kila mtu kwa mpangilio wake na kukosa ladha halisi kwa watu wanaotutazamaπ.
Binafsi nipo pembeni kwenye hii ngoma inayopigwa na watu ambao kwao Ni furaha kutokana na uchezaji wa watu wanaowapigia hii Ngoma kuicheza bila mpangilio nakuonekana Kumbe hawajui Asili ya Mdundo huo kwao Ni kituko na wanawaona "Weupe Tu".
Naukumbuka Ule usiku wa Klabu Bingwa pale Jijini "Casablanca, Morocco π²π¦" katika hatua ya robo Fainali msimu uliyopita Dhidi ya Wydad Casablanca Simba SC Tanzania wanacheza Mechi ya kiume Sana chini ya Kocha Robertinho hakuna mtu aliyetarajia K**a mfalme wa Jiji la Casablanca akiomba mungu mpira japo uishe wajaribu kupata ushindi kwa njia ya mikwaju ya Penati Asubuhi na mapema watu wanajazana pale "JNIA" Kuipokea Simba huku Robertinho' akionekana Ni shujaa Sana.
Ilikuwa Ni mbinu za kiufundi na siyo bahati akiwa ameikuta Timu katikati mwa msimu ikiwa Hakuna pendekezo la mchezaji wake hata mmoja anavunja uteja mbele ya watani zetu Yanga ambao Before tulikuwa wateja zao....hapa naomba nieleweke simpi sifa kwakuifunga Yanga Bali alirejesha Heshima kwa Klabu na watu wake Hususani kwenye Dabi.
Anaenda kumaliza Ligi Kuu bila kupoteza Mchezo wowote Timu ikiwa na displine kubwa wachezaji muhimu wakiandamwa na Majeruhi bado anafosi kete zake vizuri tunamaliza Ligi nyuma ya Yanga mbele ya Azam tukiwa nafasi ya Pili huku ikiwa Ndiyo Timu pekee iliyofunga na kutengeneza nafasi nyingi msimu uliyopita.
Ndio yeye Robertinho' ambaye Tumeamua kuucheza Mdundo wa Ngoma "Hatumtaki"
Ukimuuliza shabiki huyu anayesema Robertinho' aondoke Ni kwasababu gani.....? Atakwambia "Timu haichezi Vizuri" Mgumu kufanya Sub" Hana Rotation"
Mtu huyu siyo kwamba majibu hayo anauhakika nayo, Bali ameamua tu kuicheza Ngoma ambayo hajui Asili ya Mdundo wake na hamjui mpigaji.
Suala la Rotation kwenye Timu linahitaji muda ili mchezaji aingie kwenye falsafa ya mwalimu taratibu, Timu kucheza vizuri inategemea na Aina ya Mechi inahitaji Nini, Kwa mfano Mechi ya Jana Simba waliingia kwa mkakati yakuitafuta hatua ya makundi tu iwe sare au ushindi kwasababu Mpinzani tayari kwake alishaharibu na kilichobaki kwao ilikuwa Ni kujilipua K**a njia yakuitafuta Bahati na wameshindwa K**a suala la kufanya "Sub" yeye ndio alimnyanyua Captain Rafael Bocco na kumtoa Baleke' naamini wengi mliikosoa Ile sub lakini Leo hii wote Mnajuwa kilichotokea baada ya sub Ile.
Ngoma inapigwa na mpigaji hatumuoni lakini katika Hali ya kushangaza tunaicheza bila kujuwa mlio unatoka wapi na Nani anapiga hiyo Ngoma.
Amkeni Mashabiki wa Simba huo Ni mtego kwenu kwa watu ambao washaona Simba Ni ngumu kuifunga chini Robertinho' ukijitahidi Sana sare otherwise ufungwe iwe kwa matuta au ndani ya dakika 90'.
Leo hii shabiki wa Simba unaingizwa mkenge na watu wanaojifanya Ni Simba wengine juzi tu hapa tumetoka kuwashtukia agenda yao kuisema Simba Benchi la ufundi ili kuleta mfarakano na wao wapate kuishinda hii Vita mapema.
Mwalimu tunayemkataa ndio huyo Hadi Sasa kashabeba Ngao ya Jamii ambayo Watani waliitaka kwa udi na Uvumba, Mwalimu tunayemkataa ndio huyo Hadi Sasa hajapoteza Mchezo wowote wa Ligi Kuu yupo nafasi ya 3 ndani ya Mechi 3 tuna alama 9 tukiwa sawa na huyo anayeongoza Ligi.
Binafsi nimesikitika Sana kuona Hadi Kurasa zinazo sapoti Simba Leo hii wanashinikiza Robertinho' afukuzwe aletwe Nabi, Sasa nabi K**a kocha mzuri kwanini kaondolewa mapema TU kwenye hii Michuano ya Klabu Bingwa?
Mnataka Timu icheze K**a wanavyocheza Yanga, kwani Robertinho' na Gamond walisomea Ukocha sehemu moja?
Msichokijuwa katika mpira kila mwalimu anafalsafa yake ya uchezaji, Pep Guadiola hawezi kucheza K**a Zidane, Jose Mourinho hawezi kucheza K**a Arsenal Wenger, Lakini makocha hao wote wanamafanikio na kila mmoja akishinda kwa style yake, kesho na kesho kutwa Robertinho' atafukuzwa atakuja mwalimu mwengine atacheza mnavyotaka Mashabiki lakini atafungwa Sana na atakosa Mataji Kisha mtalaumu Tena Bora Timu ipate Matokeo kuliko kufungwa huku Unacheza vizuri.
Amkeni Mashabiki wa Simba Bila ya Hivyo hii Ngoma mtaicheza Wenyewe, Ni Mimi MOUD Mtanzania