05/04/2026
TAIFA MOJA, KURA MOJA: TUIWEKE TANZANIA KILELENI KATIKA TUZO ZA WORLD TRAVEL AWARDS 2026
Tanzania imeingia kwa kishindo katika tuzo za kimataifa za World Travel Awards - Africa 2026 ikiwa imeteuliwa katika vipengele nane (8) muhimu. Hii ni fursa nyingine ya kudhihirisha kuwa sisi ni kitovu cha utalii barani Afrika.
Kama mdau wa utalii, nawaomba tushirikiane kuipigia kura nchi yetu katika vipengele hivi:
Hifadhi Bora ya Taifa: Serengeti
Kivutio Bora cha Utalii: Mlima Kilimanjaro
Hifadhi Yenye Mandhari Bora: Nyerere
Hifadhi Bora ya Utamaduni: Katavi na Ruaha
Sehemu Bora kwa Fungate (Honeymoon): Kitulo
Paradiso ya Tembo Afrika: Tarangire
Hifadhi Bora ya Milima: Arusha, Kilimanjaro, Udzungwa, na Mahale
Hifadhi Bora ya Wanyama Wakubwa Watano (Big 5): Nyerere na Serengeti
Jinsi ya Kupiga Kura:
Muda ni kuanzia tarehe 30 Machi hadi 17 Julai 2026.
Tembelea: www.worldtravelawards.com/vote
Jisajili (Register) kwa kutumia jina, email, na password.
Hakiki email yako (Verify email) kupitia inbox yako.
Chagua Africa na upige kura kwa Tanzania katika vipengele vilivyotajwa. Pia unaweza ku-scan QR Code iliyo kwenye picha ili kufika kwenye ukurasa wa kupiga kura moja kwa moja.
Kura yako moja ina nguvu ya kuitangaza Tanzania duniani kote. Tushirikiane kuiweka bendera yetu kileleni.