Utalii wa Ndani

Utalii wa Ndani Utalii wa ndani ni Mradi/ Project ya kuhamasisha utalii wa ndani Tanzania, iliyo chini ya NGO iitwayo JIAJIRI - The Greenlife Network.

Ungana nasi katika kuhamasisha ukuaji wa sekta hii. Tembelea vivutio vyetu, Jivunie nchi yetu. Tanzania ni kati ya Nchi chache zenye vivutio vingi vya kitalii Duniani, watu wengi kutoka Ulaya, Amerika na Asia nk wamekuwa wakisafiri kwa umbali mrefu kufika Tanzania kwa ajili ya kuviona vivutio hivyo, idadi ya wageni imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Baadhi ya vivutio hivyo ni Mlima Kilimanja

ro,Ngorongoro Crater,hifadhi za Serengeti, Tarangire, Manyara, Mikumi, Ruaha, na nyingine nyingi, miji mikongwe ya Bagamoyo, Kilwa, Zanzibar nk, Mabonde, Mito,Maporomoko, mapango na vitu vinginevyo vingi vilivyomo sehemu mbalimbali za Tanzania. Pamoja na uwepo wa vivutio hivi nchini, ni watanzania wachache sana wanaovifahamu, wengi wetu tumekuwa tukifikiri kwamba vivutio hivyo vipo kwa ajili ya wageni kutoka nje na hivyo kutokujishughulisha navyo kabisa, na wengine wanadhani ni ansa kutembelea maeneo hayo. Tunawahamasisha watanzania kubadili tabia kwa kujijengea utaratibu wa kutembelea maeneo haya yenye vivutio kila wakati, kwani ni njia mojawapo ya kufurahia maisha na pia kujifunza vitu mbalimbali katika maeneo hayo na hivyo kuongeza hali ya kujivunia nchi yetu na kuipenda kwa dhati.

NI UTAMADUNI, UNAENZIWA, NI UTAMBULISHONa Nkungu Hango 30.06.2025UTAMADUNI ni mkusanyiko na muunganiko wa namna jamii fu...
30/06/2025

NI UTAMADUNI, UNAENZIWA, NI UTAMBULISHO

Na Nkungu Hango 30.06.2025

UTAMADUNI ni mkusanyiko na muunganiko wa namna jamii fulani inavyoishi katika maisha yao.

Katika tamaduni kuna mambo ya msingi yanayoibeba na kuitambulisha jamii husika ambavyo ni mila na desturi katika imani zao, mavazi na uvaaji wake, chakula na ulaji wake, uzalishaji wa mali, ndoa na uoaji wake, ngoma na nyimbo zao, michezo yao, uongozi na ufanyaji wa maamuzi yao na mengineyo yenye kuakisi jamii fulani.

Ni kweli utambulisho wa jamii fulani hutokana na utamaduni wao.

Kuna misemo inasema, ukipoteza utamaduni wako, umepoteza utambulisho wako.

Uimara wa utamaduni katika jamii fulani ndiyo msingi wa uimara wa kukuza maendeleo kulingana na nyakati na mabadiliko katika nyanja tofauti za kijamii, kiuchumi, kiuongozi(kisiasa), kiutamaduni na kimazingira.

Kwa sasa baadhi ya jamii zimebadilika kutokana na sayansi na teknolojia, mabadiliko hayo ya sayansi na teknolojia hayajafanya jamii hizo kutokukumbatia utamaduni wao bali misingi yao ya kiutamaduni wameiingiza huko na kuiendeleza kisayansi na kiteknolojia bila kupoteza asili na ladha yao.

Mdau wa Nkungu Hango, Mtaalam Mwandamizi katika Sekta Fedha, Emmanuel Gyuzi, anasema " "Sio jamii za Kihindi tu zinazohifadhi mila hata kwa jamii zingine za Ulaya zinafanya hivyo.

Mathalani nilikuwa masomoni Uholanzi Chuo nilichosoma Erasmus University walikuwa na Programme nyingi tu za kutuletea mafunzo ya uasili wa Uholanzi Kuanzia vyakula na ulaji wake, utengenezaji wa chizi na ngoma zao za asili vile vile kulikuwa na programme za kututembeza kwenye site za makumbusho yao mbalimbali ili kujionea utengezaaji vitu vya asili k**a vIatu vya mbao ambavyo mababu zao walivaank..."

Kuna nguli aliyekuwa mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hayati Ali Mufuruki, amewahi kusema kuwa Utamaduni ni bidhaa ya kibiashara inayokua kwa kasi ikiwa imekubatia utajiri mkubwa uliohifadhiwa huko ambao jamii inatakiwa kuwekeza eneo hilo.

Kwa mantiki hiyo, Mufuruki alikuwa anaiasa na kuikumbusha jamii kutambua katika tamaduni zetu kuna utajiri, ijitazame namna ilivyohifadhi utajiri huo, na itafute namna ya kuuwekeza utajiri huo ili uzalishe mapato.

Nikishabihisha maneno ya Bw. Gyuzi na Bw. Mufuruki, unaweza kuiangalia nchi k**a Brazil jinsi inavyofanya vizuri katika kunufaika na utamaduni katika nyanja tofauti ikiwemo sherehe za kitaifa na kimataifa za kitamaduni za samba na nyinginezo.

Tukienda Uchina tunashuhudia wakati usherekeaji wa sikukuu zao, masuala ya kitamaduni ndiyo hushika hatamu katika unogeshaji wa sherehe zao kuanzia mavazi, chakula, ngoma, mapambo, michezo nk.

Kumbuka Wachina wana namna ya kuadhimisha mwaka wao wa Kichina, ni tukio kubwa ambalo Wachina duniani kote hufanya sherehe na inasherehekewa kweli kweli, Mchina akikosa tukio hilo hujihisi katenda kosa kwa nchi yake.

Na nchi za Ulaya karibu zote zinaenzi utamaduni wao nje ya kuwa na utamaduni wa kisasa.

Unaweza kukumbuka mazishi na maziko ya Malkia, Elizabeth yalitawaliwa na masuala ya kitamaduni pia hadi mwili wake ukienda kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele, tukio hilo lilikuwa la kitamaduni lililopelekea wageni waliohudhuria kuzuia kuingia huko kwenye usiri wa kitamaduni (mirimu).

Hata Rais wa Marekani, Joe Biden alizuiwa kuhudhuria tukio hilo la kimila lililofanywa na wahusika tu.

Hata hivyo, Waingereza wote walikuwa wanafuatilia kwa umakini hiyo hatua wakisubiria nje ya Kasri la Kifalme/Kimalkia.

Hapa hatuwezi kusahau matumizi ya maua, bila kununua maua kwenda kuweka kwenye kaburi au mahali maalum palipotengwa itakuwa hujakamilisha maombolezo yako.

Ni utamaduni, unaenziwa, ni furaha na utambulisho wao.

Tukiwatembelea Wahindi, hawa nao wanatupa somo kupitia sherehe za LIWALI ambao Wahindi huazimisha tukio hilo popote walipo wakifungamanisha na ibada za Miungu wao.

Hapa tuangalie malighafi zinazotumika kufanikisha tukio hilo, kiasi gani tukio linaweza kutoa kipato kwa jamii husika.

Nje ya hapo tukio limezalisha umoja, upendo, kukuza imani, mshik**ano, kukuza uchumi, kujenga nguvu ya pamoja na matokeo yake ni uzalendo halisi wenye fungamano na uasili wa Miungu wao.

Nisikupoteze, kumbuka hizi ni tamaduni zenye kuendana na usasa na zinaandaliwa kisasa lakini zimetimiza utamaduni wao wa asili katika usasa au dunia ya leo.

Nikirejea kwetu, utamaduni uko wapi, unaenziwa wapi, bidhaa yake imetambuliwa kiasi gani, nguvu yake iko wapi katika maendeleo na mshik**ano? Tumepoteza.

K**a tulivyoona hapo juu, utamaduni unaileta jamii pamoja, kuiunganisha kuwa na nguvu moja.

Tukitazama hapa kwetu, ni makabila mangapi ambayo bado yanaunganishwa na utamaduni wao na kishik**ana ipasavyo k**a watoto wa mama mmoja.

Bila shaka kila mmoja atakumbuka Wasaai k**a vile wao ndiyo wamezaliwa wakikumbatia utamaduni wao pekee.

Hata watu wengine, wakienda nje ya nchi, wakiambiwa tuonyeshe utamaduni wenu, utashangaa Mnyiramba, Mnyaturu, Mnyaisanzu, Mgogo, ataruka kimasaai na kuivaa kimasaani, eti anaona fahari kwa utamaduni wa kukopa.

Ajabu lakini ndiyo kweli. Hayo makabila niliyoyataja yanawakilisha makabila mengi yaliyokaribu kupoteza uasili wake wa kitamaduni.

Tusiishie hapo, tujiulize, k**a taifa au nchi tunaurithi upi wenye kutufanya au kutuunganisha tuwe kitu kimoja katika kujivunia utaifa wa kiutamaduni.

Utamaduni ni njia ya kipekee yenye muunganiko na Mungu katika kuileta jamii pamoja yenye nguvu na uzalendo wa kujivunia uwepo wao.

Katika uongozi wa Rais, Mh Jakaya Kikwete kulianzishwa mchakato wa kupata Vazi la Taifa ili libebe utambulisho, ila kwa sasa ni zaidi ya miaka 10, bado hakuna Vazi la Taifa, usishangae kwa sababu utamaduni wetu haujapewa kipaumbele kwa sababu wanaoendeleza utamaduni wao walisema wetu ni wa kishenzi.

Ni rai yangu, kwa siku zijazo Utamaduni utakuwa ni bidhaa inayozalisha uchumi k**a tunavyoona kwa wenzetu, nasi tuamke tuanze au tuendeleze kuenzi utamaduni wetu ili tuweze kuwa na utambulisho wetu na kuondokana na dhana kuwa utamaduni wetu ni wa kishenzi.

K**a taifa lenye makabila mengi, hakuna budi, nchi ijikite kuainisha mambo ambayo yanatuweka pamoja k**a vile VAZI LA TAIFA ili tuwe na utambulisho rasmi nk.

Pia kila kabila liwajibike kuirejesha jamii yake katika misingi ya kitamaduni ili liweze kurithisha asili yake kwa kizazi kijacho.

Ni aibu utamaduni wa jamii fulani kufa kisa kukumbatia utamaduni wa kigeni ambao wenye utamaduni wao wanaukumbatia, kuulinda na kuuenzi kwa wivu mkubwa, ukiambatana na imani za kiroho.

Picha: Hisani ya Mitandao

Piga kura kwa Simba dhidi ya Fenerbache
28/04/2023

Piga kura kwa Simba dhidi ya Fenerbache

“🏆 ”

Tafakuru 🤔
28/06/2022

Tafakuru 🤔

African Queen, Tanzania
16/06/2022

African Queen, Tanzania

24/04/2022
Makumbusho ya Mkwawa katika eneo ilipokuwepo ngome yake iliyokuwa imezungukwa na ukuta wa mawe wenye umbali wa KM 13 na ...
15/12/2019

Makumbusho ya Mkwawa katika eneo ilipokuwepo ngome yake iliyokuwa imezungukwa na ukuta wa mawe wenye umbali wa KM 13 na urefu wa futi 12.

KALENGA

Sitoi KURA yangu kwa mgombea asiyekuwa na mipango madhubuti juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,  . Nkungu Han...
15/11/2019

Sitoi KURA yangu kwa mgombea asiyekuwa na mipango madhubuti juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, . Nkungu Hango.

Hongera sana kwa Taifa Stars kwa kututoa kimasomaso... historia mpya mmeandika baada ya miaka 39.. Utalii wa kihistoria ...
24/03/2019

Hongera sana kwa Taifa Stars kwa kututoa kimasomaso... historia mpya mmeandika baada ya miaka 39..

Utalii wa kihistoria Leo National Stadium, Dar es salaam. Tanzania

Ni siku ya kipekee Leo... usiombe kukosa
24/03/2019

Ni siku ya kipekee Leo... usiombe kukosa

Utalii wa ndani Leo ni National Stadium... KILA la kheri Taifa Stars
24/03/2019

Utalii wa ndani Leo ni National Stadium... KILA la kheri Taifa Stars

Address

Dar Es Salaam
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Utalii wa Ndani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category