30/06/2020
FINALLY I FOUND THE WOMAN I WANTED
Dear mwanamke nkutakae najua na naamini unajitambua, hakuna mwanaume anayetaka mwanamke asiyejitambua, mwanamke asiye na maono ya mbeleni, mwanamke anayewaza iphone x wakati anaka chumba kimoja mwananyamala, mwanamke ambaye anapenda wigi kuliko kulipa kodi na kujinyima kwa ajili ya hatari zinazoweza kutokea mbeleni.
Dear manamke nikutakae, wewe ni kitu cha dhamani sana kwangu, wala sitoacha hata siku moja moyo wako na mapigo yaende mbio kwa kuniwaza mimi, bali nitakufurahisha kila mara hata mapigo ya moyo yapungze speed.
Dear mwanamke nikutakae, Tambua kuwa mwanaume unayempata amekwisha kuumizwa na wanawake wengine wasio na busara wala huruma k**a wewe, hivyo jitahidi kumbadilisha, maana maumivu huaribu moyo, vidonda alivyonavyo ni vikubwa, ni vichafu, vinatoa usaha, nakuomba mwanamke nikutakae, tafuta spririti na iodin solution uanze kuvisafisha na kufanya tiba kabla ya lolote lingine, najua wewe ni daktari wa familia yako k**a tulivosema hapo awali, naamini utatibu makovu yote hata asione wala kukumbuka k**a alishawahi kuumia hapo.
Tafadhali mwanamke nikutakae, kaa chini na utafakari, siji kwako kwa sababu wewe ni mweupe wala kwa kuwa wewe una makalio makubwa, nakuja kwako kwa kuwa wewe ndie nikutakae, nakupenda k**a ulivo, hivyo usisubutu kukaa saluni na vibarazani na kuanza kutafuta sifa mpya ambazo hukuwa nazo mwanzo.
Dear mwanamke nikutakae, rangi yako ni nzuri kuliko ya mwanamke yeyote ambaye nimewahi kumuona hapa duniani, maneno haya yanatoka moyoni, kujaribu kujipaka vipodozi vya kukuchubua na kuchuna ngozi yako ili uonekane mweupe ni kunifumba macho yangu na kunifumbua kwa wengine, nikutaka kuonekana k**a ndizi mbivu za kuchoma katika vidole na miguuni, tafadhali mwanamke nikutakae usifanye chochote katika ngozi yako kwani kubadili muonekano wako ni kupunguza hamu niliyokuwa nayo kwako hapo awali.
Dear mwanamke nikutakae, kumcha mungu ndio chanzo cha maarifa, usichoke kuomba na kufunga, kwani ukitaka familiya yako na ndoa yako iwe salama pakukimbilia ni kwa mungu. @ Akiliyapesa