Adolphina - Camp Hotels Limited.

Adolphina - Camp Hotels Limited. Joshua Real Estate limited

04/09/2026

WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI AMANI GOLUGWA

SEHEMU 11.

MAHAK**A INAREJEA

1. Majaji wamerejea Mahakamani.
2. Mheshimiwa Lissu yupo Mahakamani.
3. Shahidi Amani Sam Golugwa yupo Mahakamani.
4. Mawakili wa Serikali wote wamefika na wapo tayari.

MAJAJI WANATETA KIDOGO

Jaji Ndunguru: Naomba tuendelee.

Ajuaye Zegeli: Mheshimiwa Jaji, tupo tayari kuendelea na Mshtakiwa yupo. Shauri linakuja kwa ajili ya maswali ya dodoso. Tunaomba tuendelee.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?

Lissu: Nipo tayari.

Shahidi anapanda kizimbani.

Jaji Ndunguru: Shahidi, upo tayari?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Tuendelee na cross-examination, lakini pia shahidi, kiapo chako kinaendelea.

Nassoro Katuga: Sasa, Shahidi, tuendelee tulipoishia. Ila, Bwana Shahidi, tufute yale mambo ya wakili mwenye roho mbaya.

Golugwa: Sawa, tuendelee.

Nassoro Katuga: Shahidi, unakumbuka tulikuwa tunazungumzia taarifa ya SADC?

Golugwa: Nilikuwa bado sijaeleza vizuri.

Nassoro Katuga: Naomba upokee taarifa ya SADC, utuonyeshe ni wapi wameandika kwamba mash*taka ya Mwenyekiti ni ya uongo.

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, naipokea, lakini kuna maelezo. Ameninukuu vibaya. Mimi nilisema kwa ripoti ya uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi na taarifa mbalimbali za UN.

Sasa ananiuliza peke yake kuhusu taarifa ya SADC.

Nassoro Katuga: Sasa nionyeshe ni wapi katika taarifa ya SADC walipoandika ni uongo.

Golugwa: (Anasoma)

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji ni wapi katika hayo maneno kwamba Tundu Antipas Lissu amesh*takiwa kwa kesi ya uongo.

Golugwa: Katika haya maneno kuna sehemu wamemtaja Tundu Lissu na kesi yake.

Nassoro Katuga: Sasa tueleze ni wapi wamesema kwamba Tundu Lissu amesh*takiwa kwa kesi ya uongo.

Golugwa: Sasa amenibana nionyeshe katika taarifa ya SADC, wakati mimi nilieleza taarifa mbalimbali.

Nassoro Katuga: Hayo maneno kwamba Tundu Lissu amefunguliwa kesi ya uongo yamo au hayamo?

Jaji Ndunguru: Shahidi, jibu swali. Maneno hayo yapo au hayapo?

Golugwa: Maneno hayo kwamba kesi ya uongo hayamo.

Nassoro Katuga: Umesema hayo maneno humo hayamo, ila unasema yapo katika kesi ya UN?

Golugwa: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Hiyo ripoti ya UN tuambie inaitwaje.

Golugwa: Ripoti ya Kamisheni ya UN ya Haki za Binadamu.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo Kamisheni ya UN ya Haki za Binadamu ilikuwa ni waangalizi wa uchaguzi mwaka jana?

Golugwa: Hapana.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo umeshindwa kututajia ripoti gani ya waangalizi imetaja kwamba hii ni kesi ya uongo.

Golugwa: Nimetaja katika taarifa mbalimbali za waangalizi wa uchaguzi.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo huu ushahidi kwamba kesi ni ya uongo ni ushahidi wa kusikia?

Golugwa: Ni ushahidi wangu, nimesoma. Hata mimi najua ni kesi ya uongo.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo haya maneno, “amesh*takiwa kwa kesi ya uongo,” umeshindwa kuyaonyesha hapa Mahakamani?

Golugwa: Si kweli, nimeonyesha katika ripoti ya SADC.

Nassoro Katuga: Basi tuhame huko. Tuambie, unajua au hujui Tanzania ni nchi huru?

Golugwa: Najua ni nchi huru.

Nassoro Katuga: Imekuwa huru tangu lini?

Golugwa: Tangu 9 Desemba 1961.

WEKA EMOJI K**A UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI

16/05/2026
10/07/2024
Wewe endelea kukaa kwa ndugu nakusubiri chai na mkate turakutana uzeeni
26/05/2024

Wewe endelea kukaa kwa ndugu nakusubiri chai na mkate turakutana uzeeni

Address

P. O. Box 45466
Dar Es Salam
MTAKUJASTREET,ILALADSM

Telephone

+255788189018

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Adolphina - Camp Hotels Limited. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share