Sasafari Tanzania

Sasafari Tanzania Ruaha Mikumi Udzungwa Serengeti Tarangire Ngorongoro Manyara Saadani Kilimanjaro parks

We are tour

Ruaha Mikumi Udzungwa Serengeti Tarangire Ngorongoro Manyara Saadani Kilimanjaro parks

We are tour company based in Dar es salaam mikumi&Iringa Tanzania.

Hatima ya Ndegewa Tunduni 🌿By Zenyumbuz. (Santiago)Kulikuwa na mama ndege aliyependwa sana na watoto wake watatu. Kila s...
23/11/2025

Hatima ya Ndegewa Tunduni 🌿

By Zenyumbuz. (Santiago)

Kulikuwa na mama ndege aliyependwa sana na watoto wake watatu. Kila siku alitoka mapema kwenda kutafuta chakula ili kuwalisha na kuwalinda dhidi ya hatari za msituni. Alijua kuwa watoto wake bado wadogo sana na walitegemea kila kitu kutoka kwake.

Siku moja, asubuhi yenye ukimya na upepo mwanana, mama ndege aliruka kwenda k**a kawaida kutafuta chakula. Hakujua kuwa wawindaji walikuwa wameingia msituni wakiweka mitego yao kwa wanyama wadogo. Akiwa anajaribu kukwepa hatari, alinaswa na hatimaye kuuawa bila huruma.

Jua lilipanda juu, watoto wake wakasubiri… na kusubiri. Walijua mama hurudi kabla jua halijawaka sana, lakini safari hii hakutokea. Njaa ikaanza kuuma, hofu ikaanza kutanda, na sauti za misitu zikaanza kuwatisha.

Lakini hapa ndipo simulizi linageuka…

Katika mti jirani aliishi tai dume, ndege mkongwe ambaye siku zote aliangalia jinsi mama ndege alivyowalea watoto wake kwa upendo mkubwa. Aliona siku hiyo alivyotoka, na baadaye akasikia kelele za wawindaji. Alipokwenda chini kwa tahadhari, aligundua kilichotokea.

Tai dume alirudi kwenye mti na kuwaangalia watoto waliokuwa wakilia bila msaada. Alijua si damu yake, alijua si wajibu wake — lakini pia alijua kuwa ndicho kilichokuwa cha haki.

Akaruka juu ya tundu na kusema kwa sauti tulivu,
“Watoto, hamko peke yenu.”

Kutoka siku hiyo, tai dume akawa mlezi wao. Alileta chakula, aliwalinda dhidi ya hatari, na polepole akawafundisha kuruka. Hawakusahau mama yao, lakini walijifunza kuwa dunia ingawa ina giza, bado ina watu au viumbe wenye moyo wa huruma.

Wakati watoto walipokuwa tayari kuruka wenyewe, tai aliwaambia:
“Fanyeni wema mnapoweza. Msikubali mabawa yenu yawe ya ubinafsi. Mama yenu angependa muishi hivyo.”

Na kweli, walipopata familia zao baadaye, waliwalea kwa upendo ule ule waliouona.

🌟 Funzo kuu la simulizi

Wema hauhitaji uhusiano wa damu.

Dunia ina maumivu, lakini huruma ya mtu mmoja inaweza kuokoa kizazi kizima.

Majukumu ya kweli hutokana na moyo, si ulazima.

Kila kizazi kina nafasi ya kuendeleza wema walioupokea.

Nawaza tunapata wapi roho ya kishetani kuliko shetani  mwenyewe? Tunawezaje kutoa uhai wa mtu k**a sisimizi na hatush*tu...
16/11/2025

Nawaza tunapata wapi roho ya kishetani kuliko shetani mwenyewe? Tunawezaje kutoa uhai wa mtu k**a sisimizi na hatush*tuki? Kwa nini haturudishi moyo nyuma na kusema tumekosea tusameheke?

Yaani tunasema tuwasamehe wakati sisi ndio tumekosea?
Au wenzangu mmeshagundua hakuna hukumu siku ya kifo chetu???

Alhamdulilah! Nimefanikiwa kuirejesha Account  hii! Poleni sana ndugu zangu kwa sintofahamu iliyotokea.Dada yangu   mung...
07/11/2025

Alhamdulilah! Nimefanikiwa kuirejesha Account hii! Poleni sana ndugu zangu kwa sintofahamu iliyotokea.
Dada yangu mungu akupe umri mrefu najua ulipost kwa sababu ya mapenzi mema na nchi yako na kutambua utu wetu.
Wahuni hawakosekani walichokifanya hakikubaliki na lengo lao ni kufifisha jitihada unazofanya.
Kwa ndugu zangu na rafiki zangu poleni kwa taharuki.

21/10/2025

Kusafiri kunafungua kurasa zilizofungwa.

Jiwe walio likataa waashi.
24/09/2025

Jiwe walio likataa waashi.

Ninayo furaha kukutana na ndugu yangu wa siku nyingi Balozi  wa Tanzania  nchini Botswana 🇧🇼
20/09/2025

Ninayo furaha kukutana na ndugu yangu wa siku nyingi Balozi wa Tanzania nchini Botswana 🇧🇼

Kutoka dimba la Obed Itani hapa Francis  Town Simba vs Gaborone United.
20/09/2025

Kutoka dimba la Obed Itani hapa Francis Town

Simba vs Gaborone United.

Ubaya Ubwela, kila la kheri watoto wa msimbazi weekend  hii.
14/05/2025

Ubaya Ubwela, kila la kheri watoto wa msimbazi weekend hii.

10/01/2025

Address

Rwegasore Road
Morogoro
137

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sasafari Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category