Kilimanjaro-Serengeti Tours &Travels Ltd

Kilimanjaro-Serengeti Tours &Travels Ltd Lifetime memories. Choose or combine: Kilimanjaro tours

18/01/2025

UTOFAUTI YA WATU WA DAR NA WATU WA MKOANI NI HUU

Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajash*tuka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu k**a hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anak**ata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine k**a tunavyotaka kutendewa.

Share na wengine

This is the right time to plan for your next Holiday. Contact us now for more details.
12/01/2025

This is the right time to plan for your next Holiday. Contact us now for more details.

10/10/2024

Wapendwa wananchi, kwa taarifa yako: *Ilani ya Usalama wa Juu:* Tafadhali fahamu kuwa kuna kundi la watu wanaokwenda nyumba kwa nyumba wakijifanya kuwa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Wana hati na barua kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani na wanadai wanahitaji kuthibitisha kuwa kila mtu ana kitambulisho halali kwa sensa ijayo. Kumbe wanataka kuiba nyumba yako. Wako kila mahali na wanaonekana maridadi. Mtu atakuja nyumbani kwako na kusema *Nataka kuchukua picha/alama yako ya vidole kulingana na mpango fulani*. Wana kompyuta ndogo, mashine ya biometriska na orodha ya majina yote. Wanaonyesha menyu na kuuliza habari hii yote. Tafadhali kumbuka kuwa hakuna mpango k**a huo wa serikali. Tafadhali fahamu kuwa haya yote ni bandia. Usiwape taarifa yoyote. Wasiliana na Mjumbe au Watu wa Serekali ya Mtaa unaoishi k**a wana taarifa la kuwepo hilo zoezi. Kila mtu anahitaji kuwa macho na *kufahamu*!

Tuma hii kwa vikundi vyako vyote vya jumuiya. Tafadhali wajulishe familia yako na marafiki.

**Be warned*

**Nimeituma K**a nilivyoipokea

09/10/2024

Prof. Minzi na wengine!

Sijui k**a waafrika kuna siku tuta endelea na kufanikiwa k**a wenzetu wazungu, wahindi, wachina, waarabu, nk. We seem to be at the lowest thinking, intellectual and moral level. Kwa nini nasema hivyo?

Nimewekeza hela nyingi sana kununua mashamba Mkoa wa Rukwa wilaya ya Kalambo about 2,000 acres.
Nimeajiri na nalipa mishahara mizuri kila mwezi for the second year! Sijaweza hata kuvuna kuanza kurudisha hela nilizowekeza. Wanapata malazi na chakula bure nje ya misharaha yao kwenye kambi ambayo nimejenga nyumba kadhaa, nimewekeza matrekta ya kilimo na mwaka huu ilikuwa tulime 500 acres kwa kuanzia. mafuta wanatumiwa, fedha za matumizi madogo madogo wanatumiwa, viongozi ni watu wazima wa elimu ya chuo kikuu nikifikiri natoa ajira kwa waafrika wenzangu. Wapo wafanyakazi k**a 50 wote kila mwezi wana mishahara na kula na kulala bure kwani ni mbali na mjini.

ฤฐli kusimamia nilimweka mtoto wangu wa kiume asimamie baada ya masomo ya diploma, nikamwondoa baadaye aweze kupata exposure kwenye miradi mingine. Nilimweka mpaka mchungaji rafiki yangu wa siku nyingi awe anatupia jicho la pembeni kwenye kijiji cha jirani na namlipa allowance kwa mwezi ila sio mfanyakazi.

To my surprise, kumbe wamejenga syndicate kubwa mno kati yao viongozi na operators wa trekta na hasa baada ya kumtoa mtoto wangu kwenye kazi zingine nikimwachia uongozi kijana mwingine ambaye nilipewa na mpendwa kanisani graduate wa UDOM wa zaidi ya 5 years experience ambaye kwenye interview showed quite good command of leadership.

Kumbe kwa siri, wameanzisha vijishamba vyao wanalima kwa mafuta yangu ninayowatumia; wanalima mashamba ya wenyeji kwa hela SH. 70,000 kwa ekari na fedha wanagawana kwa siri; matrekta yangu yote mawili yameharibikia kwenye mashamba ya kulimia watu kupata hela, muda wa kulima shamba langu hawana, shamba langu nililopanga kulima 500 acres this year, Limelimwa only 50 acres na matrekta yasingeharibikia huko wangelima hekari zaidi ya 200, ambazo zimethibitishwa kulimwa; gari yangu ya shamba Canter imekatika chasis kumbe wanafanya biashara ya kubebea watu mazao, kokoto na mawe kwa kulipwa hela wanazo pocket kwa kugawana bila sisi kujua na walifanya siri kubwa.

Nilisukumwa kuomba na kufunga for 3 days last week na sasa nipo kwenye maombi ya wiki nzima ya kufunga nikizidi kuomba ustawi na mafanikio kwenye kazi za mikono yangu.

Kwenye migao yao ya fedha za siri mmoja inaelekea hakuridhika na utaratibu wa mgawanyo akiona anapunjwa, walipoona anasumbua wakamfitini na kumfukuza kazi.
Ndiye baadaye aliyeanika syndicate yote ambayo kumbe mpaka mchungaji wa pale niliyemwamini sana sana naye yumo!!!๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
Nikimuuliza mchungaji huyo, kulikoni yote haya yanayotokea na yeye akiwamo kuhusu, aliishia kuwa na kigugumizi na ameshindwa kabisa hata kujitetea amebaki kuomba samahani!!!!

Waafrika tunaenda wapi jamaniii!!!๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
Umaskini kweli utaondoka kwa kuwa na roho chafu na mbaya kiasi hiki kweli!!
Hivi k**a sio wokovu nilionao, watu k**a hao akipigwa risasi na mwekezaji mwingine k**a mimi, tutamlaumu hawa wezi, walafi, watu wasio na soni wala huruma k**a hawa kweli?

Nimejinyima miaka yangu yote mpaka uzeeni ili niweke urithi kwa vizazi vyangu, nijisikie nilipambana wajukuu waje kuanzia maisha bora zaidi ya yale tuliyoishi sisi, tunaishia kuwekeza kwa wezi vijana wasio na roho kiasi hiki.

Nimeshea hili ili k**a taifa tujitafakari tunakwenda wapi kwa kizazi hiki tulichonacho. Hawa ndio tunaowatengeneza wawe viongozi wa kitaifa, nchi itaweza kusogea kwa mentality ya jinsi hii.

Binafsi nimeamua kutafuta ku-employ Indians or Chinese kuendesha miradi yangu, nimechoka na waswahili acha waendelee kuwa vibarua na watumwa milele na laana zao.

Waafrika tusiporudi kumtafuta na kumwinamia Mungu kwa dhamira ya dhati mioyoni mwetu, laana ya umaskini na utumwa itaendelea kututafuna milele mpaka mwisho wa dunia

Nawashuhudia nyote kwamba Maombi yanafunua hata yaliyo sirini yaliyojificha. Mungu anaangalia dhamira iliyo safi mbele zake na humwekea ulinzi mja wake, kwenye hili, binafsi nimemuona Mungu akitenda.

*Copied and pasted*

Glory to God Almighty๐Ÿ™๐Ÿป๐Ÿ™๐Ÿป๐Ÿ™๐Ÿป

07/09/2024

Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili), simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma.

Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake.

Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe.

Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani".

Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!!

Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."K**a tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!"

* *

Usiunge mkono uovu leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, pengine kesho inaweza kuwa zamu yako.!!

Nafikri tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu. Umejifunza nini?

Asante kwa kusoma ujumbe huu sambazia wengine

01/09/2024

WHY MEN ARE CALLED "GROOMโ€, AND THE WOMAN โ€œTHE BRIDEโ€ ON WEDDING DAY?

Why is the newly wedded man called groom and the woman called bride? A friend of mine got tired of his wife just about six months after wedding. He complained bitterly to me about her and told me that he has concluded to break up with her; he went on to say that he was sure that he made a mistake. I did not respond immediately because I knew I must tell him that right thing, so I went home. And that is
what birth this message. Many men have broken up with their wives because they end up not being the wife that they have dreamt of. But they have forgotten that on their wedding day was when the man was commissioned for the new task.

Nobody calls the woman wife on her wedding day but bride,because it is the man that will groom his bride to become the wife.That is why the man is called โ€˜bridegroom or groomโ€™ and the word grooming has to do with patiently nurturing, teaching, tending and helping someone to become what he or she should be.It is therefore believed that a man that takes a woman to the altar of marriage is matured enough to patiently groom his bride to become the wife.

The man is not supposed to just expect the bride to automatically become the wife, she must be groomed. It is clear that many of us men have unnecessary expectations when we are getting married, we want some magic to happen to our wives, we want them to become what we have had in mind about who we want our wives to be; not considering the fact that the woman does not know what is on your mind except you teach her.

Our expectations are often too unrealistic, because we donโ€™t remember that change takes time and we can only expect something from someone that knows what we want. So before you think of breaking up, have you groomed her? Have you given her time to understand you? Hope you realize that a turtle will never become a hawk? God often brings people that are opposites of each other together in marriage so that they can help each other in their place of weaknesses.

If your wife is weak where you are weak, then where will you get the strength that is needed? The problem with many of us is that we donโ€™t accept people before attempting to change them. Of course, our wives are not from our backgrounds, so it will take time for them to adjust. Stop trying to change her, accept her, love her, teach her and be patient with her; that is what grooming is all about. She is going to be your wife but she is your bride now, so groom her.

Stop complaining about her, she may be a turtle and you a hawk, she cannot fly so be patient with her. I donโ€™t believe that your marriage canโ€™t work, be patient and allow God to help you.

Share this master piece to bless someone ๐Ÿ™
๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ๐ŸŒธ

07/08/2024

ALIEZALIWA MIAKA YA 1960, 1970, 1980
TUINUE MIKONO YETU JUU NA KUMSHUKURU MUNGU

KWA SABABU:- zifuatazo

1) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho kwa miaka hiyo hakijawahi kuwapigia simu marafiki kwenye simu bali ilikuwa ni kuwatembelea majumbani mwao kila wakati.

2) Sisi ni kizazi cha mwisho kuandika barua kwa wachumba wetu na wapendwa wetu na ujumbe bado ulifika.

3) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho kilicheza mpira shuleni kwa miguu mitupu na hatukuwahi kupata majeraha

4) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho kilicheza kwenye mvua na hatukuwahi kuugua.

5) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho tulikwenda msituni kukata kuni na kucheza lakini tulirudi nyumbani kwa kuchelewa na salama.

6) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho kilifanya kazi zetu za nyumbani bila msaada wa binti au dada wa kazi na wazazi wetu wetu walituamini kufua na kuosha vyombo.

7) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho tuliendesha baiskeli kilomita nyingi bila helmeti na hatukuwahi kupata madhara.

๐Ÿ˜Ž Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho tulilala bila net na tukiugua tulikunywa dawa za kutuliza maumivu kila tulipougua malaria na iliisha baada ya siku mbili.

9) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho tulikunywa uji na kipande cha mahindi ya kuchoma au kuchemshwa tu wakati wa chakula cha mchana na bado tulizingatia darasani.

10) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho kilikula kiporo cha ugali na bado hakikulalamika

11) Sisi ni kizazi cha mwisho kilichofanya vizuri shuleni bila vikokotoo, kompyuta na vitabu vya kumbukumbu.

12) Sisi ni kizazi cha mwisho ambacho tulikula, kwa kushiriki bakuli moja bila kunawa mikono na hatujawahi kuugua

13) Sisi ni kizazi cha mwisho kilichofurahia sikukuu za dini zote kwa pamoja na wazazi wetu tukila ubwabwa na nyama ya ng'ombe na tulijisikia kuridhika sana.

14) Sisi ni kizazi cha mwisho kubeba kilo 25 za mahindi kwenye vichwa vyetu hadi kwenye mashine za kusaga na hatujawahi kuhisi misuli kulegea.

15) Sisi ni kizazi cha mwisho tuliokuwa tukiwaogopa wazazi wetu na hatukuwa na tabia ya kuwajibu wanapozungumza au kukukemea na tulikua watu wa kuheshimu tamaduni zetu

16) Sisi ni kizazi cha mwisho kupigwa na mwalimu na kutoripoti nyumbani na bado tulihisi haki imetendeka

17) Sisi ni kizazi cha mwisho kuchunga ng'ombe na kushinda maporini bila kujali hatari ya wezi wa kuiba mifugo tunayoichunga

18) Sisi ni kizazi cha mwisho kusoma kitabu cha Chinua Achebe
๐‚๐‡๐ˆ๐๐”๐€ ๐€๐‚๐‡๐„๐๐„ ๐€๐Œ๐„๐€๐๐ƒ๐ˆ๐Š๐€ ๐Š๐€๐“๐ˆ๐Š๐€ ๐‘๐ˆ๐–๐€๐˜๐€ ๐˜๐€๐Š๐„ ๐˜๐€ "๐“๐‡๐ˆ๐๐†๐’ ๐…๐€๐‹๐‹ ๐€๐๐€๐‘๐“" ๐Š๐–๐€๐Œ๐๐€.
๐Œ๐ญ๐ฎ ๐š๐ง๐š๐ฒ๐ž๐ฐ๐š๐š๐ฅ๐ข๐ค๐š ๐‰๐š๐ฆ๐š๐š ๐ณ๐š๐ค๐ž ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ฌ๐ก๐ž๐ซ๐ž๐ก๐ž ๐ก๐š๐Ÿ๐š๐ง๐ฒ๐ข ๐ก๐ข๐ฏ๐ฒ๐จ ๐ค๐ฐ๐š ๐š๐ฃ๐ข๐ฅ๐ข ๐ฒ๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š๐จ๐ค๐จ๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ฎ ๐ฒ๐š ๐ง๐ฃ๐š๐š. ๐–๐š๐š๐ฅ๐ข๐ค๐ฐ๐š ๐ฐ๐จ๐ญ๐ž ๐ฐ๐š๐ง๐š ๐ฏ๐ฒ๐š๐ค๐ฎ๐ฅ๐š ๐ฆ๐š๐ฃ๐ฎ๐ฆ๐›๐š๐ง๐ข ๐ค๐ฐ๐š๐จ.
๐“๐ฎ๐ง๐š๐ฉ๐จ๐ค๐ฎ๐ฌ๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ค๐š ๐ฎ๐ฌ๐ข๐ค๐ฎ ๐ฐ๐š ๐ฆ๐›๐š๐ฅ๐š๐ฆ๐ฐ๐ž๐ณ๐ข ๐ค๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐š๐ซ๐๐ก๐ข ๐ฒ๐š ๐ค๐ข๐ฃ๐ข๐ฃ๐ข ๐œ๐ก๐ž๐ญ๐ฎ, ๐ฌ๐ข๐ฒ๐จ ๐ค๐ฐ๐š ๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ฎ ๐ฒ๐š ๐Œ๐›๐š๐ฅ๐š๐ฆ๐ฐ๐ž๐ณ๐ข.
๐Š๐ข๐ฅ๐š ๐ฆ๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐š๐ง๐ ๐ž๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ข๐จ๐ง๐š ๐ฆ๐›๐š๐ฅ๐š๐ฆ๐ฐ๐ž๐ณ๐ข ๐š๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ง๐ฒ๐ฎ๐ฆ๐›๐š๐ง๐ข ๐ค๐ฐ๐š๐ค๐ž.
๐“๐ฎ๐ง๐š๐ค๐ฎ๐ฌ๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ค๐š ๐ค๐ฐ๐š๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ฎ ๐ง๐ข ๐ฃ๐š๐ฆ๐›๐จ ๐ณ๐ฎ๐ซ๐ข ๐ค๐ฐ๐š ๐‰๐š๐ฆ๐š๐š ๐ค๐ฎ๐ค๐ฎ๐ฌ๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ค๐š ๐ฉ๐š๐ฆ๐จ๐ฃ๐š.

๐Š๐ฐ๐š ๐ก๐ข๐ฒ๐จ ๐ญ๐ฎ๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐ž ๐ง๐š ๐ฎ๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐ฐ๐ž๐ญ๐ฎ ๐ข๐ฅ๐ข ๐ญ๐ฎ๐Ÿ๐ฎ๐ซ๐š๐ก๐ข๐ž ๐ง๐ ๐ฎ๐ฏ๐ฎ ๐ฒ๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š ๐ฉ๐š๐ฆ๐จ๐ฃ๐š.
๐“๐ฎ๐ค๐ข๐ญ๐š๐›๐š๐ฌ๐š๐ฆ๐ฎ ๐ก๐š๐ข๐ฆ๐š๐š๐ง๐ข๐ฌ๐ก๐ข ๐ค๐ฐ๐š๐ฆ๐›๐š ๐ก๐š๐ญ๐ฎ๐ง๐š ๐ฆ๐š๐ญ๐š๐ญ๐ข๐ณ๐จ ๐ข๐ฌ๐ข๐ฉ๐จ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š ๐ค๐ฐ๐š๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ฎ ๐ญ๐ฎ๐ง๐š ๐ง๐ ๐ฎ๐ฏ๐ฎ ๐ฒ๐š ๐ค๐ฎ๐ฒ๐š๐ฌ๐ก๐ข๐ง๐๐š ๐ฆ๐š๐ญ๐š๐ญ๐ข๐ณ๐จ.

๐๐ž๐ค๐ž ๐ฒ๐š๐ค๐จ ๐ฎ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ญ๐š๐›๐š๐ฌ๐š๐ฆ๐ฎ ๐ฅ๐š๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ฆ๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ฉ๐š๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐ฆ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐œ๐ก๐ž๐ค๐š.
๐”๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ฉ๐ž๐ค๐ž ๐ฒ๐š๐ค๐จ ๐ฎ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐Ÿ๐ฎ๐ซ๐š๐ก๐ข ๐ฅ๐š๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ฆ๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ฐ๐ž๐ง๐ ๐ข ๐ฆ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ฌ๐ก๐ž๐ซ๐ž๐ก๐ž๐ค๐ž๐š.
๐”๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ฉ๐ž๐ค๐ž ๐ฒ๐š๐ค๐จ ๐ฎ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ญ๐š๐ฆ๐ค๐š ๐ฅ๐š๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ฆ๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ฉ๐š๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐ฆ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐จ๐ง๐ ๐ž๐š.

๐“๐ฎ๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐ณ๐ž ๐ฆ๐š๐ฆ๐›๐จ ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐จ ๐ฒ๐š๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ญ๐ฎ๐ฎ๐ง๐ ๐š๐ง๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ฉ๐š๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐ค๐ฎ๐ฅ๐ข๐ค๐จ ๐ฆ๐š๐ฆ๐›๐จ ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐จ ๐ฒ๐š๐ญ๐š๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ค๐ฎ๐ญ๐ž๐ง๐ ๐š๐ง๐š๐Ÿ™๐Ÿฝ.

19) sisi ni kizazi cha mwisho kuoga mtoni na kutembea bila viatu msituni na iliyojaa nyoka wakali

20) Na hatimaye sisi ni kizazi cha mwisho kuamka alfajiri na baridi kali bila kuvaa sweta na kwenda kukamua ng'ombe, shamba, kuchota maji kabla ya kwenda shule kwa miguu kilomita 5 na hatukuwahi kuchelewa tofauti na kizazi cha leo. .

*KUNA LA KUJIFUNZA*

C&P

22/07/2024

**
Omba Yehova Mungu akuongoze kwenye tabia njema ambazo zitavuta uwepo wake maishani mwako.
๐Ÿ”ฅ Ee Yehova Mungu, nisaidie niwe mwaminifu
๐Ÿ”ฅ Nisaidie niwe mnyenyekevu kwa wote ata wasionipenda
๐Ÿ”ฅ Naomba, achilia roho yako Takatifu ndani yangu
๐Ÿ”ฅ Fanya njia mahali nimekwama
๐Ÿ”ฅ Ondoa fitina kati yetu tukiwa eneo la kazi, ofisini, shambani Nk
๐Ÿ”ฅ Nisaidie kuomba
๐Ÿ”ฅ Nisaidie kuwatendea mema wengine
๐Ÿ”ฅ Niwe baraka kwa wengine.
๐Ÿ”ฅ Niondolee roho ya kukataliwa
๐ŸŒฑ Napokea roho ya kibali na neema juu yangu kwa jina la Yesu mwanao.
๐Ÿ”ฅ ๐ŸŒŸ Adui zangu wanaswe kwa mtego wako.
Omba zaidi na zaidi kadiri Mungu anavyokusukuma ndani yako usifungwe na hoja hizi peke
Bali tii zaidi kile Roho Takatifu itakavyokuongoza.๐Ÿ™

Hiyo miongozo inakupa ๐Ÿ’ก mwanga tu, Amen ๐Ÿ™Yohana 17:3.
* Jifunze Biblia kwa ukawaida, utabarikiwa sana!

Dhambi sikuzote ni mbaya sana! Basi mkitunga uongo kumbukeni kuwaza yajayo na muipange sawasawa!
22/05/2024

Dhambi sikuzote ni mbaya sana! Basi mkitunga uongo kumbukeni kuwaza yajayo na muipange sawasawa!

28/04/2024

WE LIVE IN VERY INTERESTING AND FUNNY TIMES (2Timothy3:1-5)

1.We live in times where we see many humans, but not humanity.

2.We live in times where the rich has more rooms than children and the poor has more children than rooms.

3.We live in times where smart phones bring you closer to those who are far, but distance you from those who are closer.

4.We live in times where we open Facebook, more than The Holy Book;

5.We live in times where a single mother can look after 10 children, but 10 children can't look after a single mother;

6.We live in times where the rich walk miles to digest food, while the poor walk miles to search for food;

7.We live in times where women are paid to be naked, while others have no clothes to cover their nakedness.

8. We live in times where our contact lists are huge, but our relationships are poor.

9. We live in times where our possessions are more, but our appreciation is less;

10. We live in times where we know how to earn a good living, but somehow forget how to live a good life;

11.We live in times where many know the price of everything, but not the value of anything.
Indeed, we live in a strange world. May God help and Guide Us

07/04/2024

HELLEN-997673
I use NALA for moneybyransfwr to Africa. It is fast and secure.

12/03/2024

Nani k**a Mama?

Address

Pasua-Relini
Moshi

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 13:00
Sunday 10:00 - 13:00

Telephone

+255682962868

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kilimanjaro-Serengeti Tours &Travels Ltd posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category