Tourism attractions in Tanzania.

Tourism attractions in Tanzania. This is all about Tanzania tourism attraction, more than 20 national parks has got alot to tell abou

15/05/2023
07/02/2021
18/01/2021

K**A UPO KWENYE BIASHARA YA UTALII SOMA HAPA

Mambo ambayo wengi huwa hawazingatii wakati wa kuandaa website ndiyo ambo ya muhimu sana kuliko yale unayohangaika nayo. Kuwa na picha au video za kuvutia wala siyo sababu ya msingi ya kukuwezesha wewe kupata wageni kupitia website yako, kupata website designer mzuri anayejua ku design website nzuri pia siyo kigezo cha muhimu sana katika kupata wageni.

Ili kupata wageni wanaofanya booking kupitia website yako ni muhimu kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo.

1. Taarifa nzuri zinazoeleweka kwa wasomaji na ziwe zimeandikwa kwa kifupi na kwa lugha rahisi, kumbuka utalii ni biashara ya ukarimu hivyo acha kuandika kiingereza k**a cha kisheria kwenye website ya utalii. Hakikisha mtu anajihisi k**a vile anaongea na mtu wakati anaposoma taarifa kwenye website yako (human language).

2. Website yako iwe inafunguka haraka. Kumbuka watu wapo busy na hawana muda mrefu wa kupoteza mtandaoni kutafuta huduma hivyo huwa hawana muda wa kupoteza kutafuta taarifa bali wanataka website zinazofunguka kwa kasi ili kuokoa muda. Kwa kipimo cha kawaida hakikisha website yako inafunguka ndani ya sekunde 5 katika mataifa ambayo unategemea kupokea wageni wako (kasi ya ufungukaji wa website unatofautiana kutoka nchi moja na nyingine kulingana na mahali server ilipo na ubora wa mtandao wa internet katika eneo husika).

3. Usalama wa website yako ni kitu muhimu sana katika kuwavutia wageni kukutumia katika safari yao. Iwapo website yako haijaunganishwa katika mfumo wa usalama wa internet (SSL Certificate / https) itawafanya watembeleaji kuogopa kwa kuhisi kuwa website yako si salama na kuna uwezekano wa kubiwa taarifa zao k**a emails na taarifa nyingine muhimu iwapo wataziweka ili kuwasiliana na wewe.

4. Upatikanaji mgumu wa taarifa muhimu. Kuna website ambazo mtu akiifungua macho yanafurahia kuiona lakini ukianza kuisoma haileweki, hupati taarifa unazohitaji kwa urahisi ingawa inawezekana kabisa kuwa zipo. Hili linaweza kiuwa tatizo kubwa maana watu hawana muda wa kupoteza kutafuta taarifa zisizoonekana kwenye website yako.

5. Website inatakiwa iongee (interractive). Unaweza usielewe lakini website inatakiwa iwasiliane na mtembeleaji na kumpa maelekezo ya nini cha kufanya. Mtembeleaji wa website hasa za utalii, anafarijika sana akiona kuwa anaweza kusaidiwa moja kwa moja na wahusika kwa kuchat (live chat support) ili kuokoa muda kwa kupata maelekezo anayohitaji ndani ya muda mfupi.

6. Tailor made products, hapa ni muhimu sana kwa kuwa inawezekana asilimia kubwa ya itineraries zako zikawa hazipendwi au hazikubaliki lakini unapompa mgeni fursa ya kujitengenezea itinerary yake mwenyewe (tailor made) inamuongezea hamu ya kutumia huduma zako.

Zipo sababu nyingi zinazokufanya ukose wageni wa moja kwa moja kupitia website yako (direct bookings) lakini kwa leo siyo mbaya uzitumie hizi kujikagua na kujua nini kimekukwamisha hapo ulipo.
Sisi Pakaya Biztech, tunatoa huduma sio tu ya kutengeneza website bali website inayokuwezesha kuonekana kwenye dunia ya internet na kukuletea wageni.

Kwa maelezo zaidi tupigie simu 0768 717785 au tembelea website yetu www.pakayabiztech.com

Address

Sanawari

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tourism attractions in Tanzania. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tourism attractions in Tanzania.:

Share

Category