17/08/2026
CHUO CHA TROPICAL INSTITUTE ARUSHA CHAFANYA ZIARA YA KIITALUMA NA UTALII JIJI LA TANGA
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Chuo cha Utalii na Usimamizi wa Hoteli TROPICAL INSTITUTE CENTRE Kilichopo ndani ya Jiji la Arusha kwa kutuamini kwa ajili ya ziara yao ya Kitaaluma na Utalii kupitia Kampuni yetu ya LIVAN CULTURAL TOURISM ENTERPRISES.
Jumla ya Wanafunzi Thelathini (30) na Walimu Watatu (3) walipata fursa ya Kutembelea Maeneo yafuatayo
Mapango ya Amboni (Amboni Caves)
Kisiwa cha Toten (Toten Island)
Historia ya Jiji la Tanga (Tanga City Historical Tour)
Hoteli ya Nyota Tano ya Tanga Beach Resort (Ziara ya Kitaaluma juu ya Usimamizi wa Hotel)
Fukwe za Bahari ya Hindi
Tunaushukuru sana uongozi wa TROPICAL INSTITUTE CENTRE ARUSHA kwa kuichagua Tanga k**a sehemu sahihi ya ziara hii ya kitaaluma
Tunaomba wakazi na wadau wa Utalii watumie chuo hiki kiwajenga vijana wao kwenye fani ya HOTELI NA UTALII.Kwa taarifa zaidi za kujiunga na chuo hiki tembelea www.tropicalcentre.ac.tz
KARIBU TANGA, TANGA RAHA