Mafia Tourism Island

Mafia Tourism Island Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mafia Tourism Island, Tourist Information Center, box 85, Mafia, Zanzibar.

31/08/2020

Mafia 2020

Mashindano ya bicycle 2020 MAFIA
31/08/2020

Mashindano ya bicycle 2020 MAFIA

Mafia Marathon 2020
31/08/2020

Mafia Marathon 2020

Mashindano ya ngalawa kisiwani Mafia
31/08/2020

Mashindano ya ngalawa kisiwani Mafia

05/08/2020
23/02/2020

Mfahamu Papa Potwe, kivutio cha utalii kisiwani Mafia Tanzania

Sambaza habari hii Email Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Whatsapp

Papa Potwe ni kivutio kikubwa kisiwani Mafia Tanzania
Je unamjua Papa Potwe? (Whale Shark) ni Samaki mkubwa duniani na huweza kufikia hadi mita 18. Akiwa mdogo huwa na kimo cha basi dogo la abiria.

Samaki hawa hupatikana maeneo machache duniani, na kwa mujibu wa watafiti wa bahari ni miongoni mwa viumbe vilivyopo hatarini kutoweka.

Moja ya maeneo wanayopatikana ni kisiwani Mafia Tanzania, sehemu nyingine ni k**a Mexico na Philipenes.

Kutokana na umuhimu wa samaki huyu wavuvi pamoja na wahifadhi wa bahari wamekua na jitihada za kuwalinda viumbe hawa.

Katika maeneo ya ufukwe wa Mafia mjini, naambiwa kuwa samaki hawa wakubwa duniani ikifika msimu wake basi huonekana hata ukiwa ufukweni, huna haja ya kuingia baharini labda tu ukitaka kuogelea nao.

Papa Potwe hujulikana pia k**a Papa mwema kwa ukarimu wake, hufuata wavuvi na watalii wakiwa ndani ya maji na hucheza nao.

Kwa kipindi cha mwaka mmoja Papa Potwe huweza kusafiri hadi kilomita 10,000.Lakini watafiti wanasema kuwa Papa Potwe wa kisiwani mafia hubaki eneo moja kwa muda mrefu. Katika makala ya National Geographic mtafiti kutoka Marekani, Simon Pierce anasema kuwa hawaendi mbali na inakua k**a wanawatembelea rafiki zao wa zamani.

''hakuna sehemu nyingi ambapo unaweza kuwaona Papa Potwe wale wale kila mara, na inakua k**a utamtembelea rafiki yako wa zamani'' anasema Simon

Humphrey Mahudi ni afisa utalii katika hifadhi ya Bahari Mafia, anasema kuwa wamekua wakishirikiana na wavuvi kuhakikisha wanawalinda samaki hawa.

''tumekua tunafanya kazi na wavuvi pamoja na halmashauri na wadau wengine kuhakikisha tunawapa mafunzo ya kuwalinda Papa hawa ambao wamo hatarini kutoweka''.

Kwa upande wa wavuvi wao wenyewe wametengeneza vikundi vya ulinzi shirikishi na jukumu la kwanza ni kuwalinda samaki hawa adimu, kutokana na asili ya samaki hawa hutembea na makundi ya samaki wengi wadogo hivyo ni fursa kwa wavuvi.

Wavuvi niliozungumza nao wanasema kuwa samaki huyu, kwao hana msimu wanamuona kila siku .

Said Isaa Kombo ni mwenyekiti wa ulinzi shirikishi kwa rasilimali za bahari na ni mvuvi, anasema kuwa mara nyingi hukutana na samaki huyu wakati mwingine wanalazimika kuachia samaki waliwavua ili tuu wampishe wala wasimdhuru samaki huyu.

''k**a akivuta nyavu zetu na asiweze kujitoa basi tunalazimika kuwasamehe wale samaki wote tuliowavua na kumuacha aende''

Mbali na jitihada zinazofanyika lakini bado Samaki hawa wanakumbwa na hatari kubwa kutokana na shughuli za uvuvi., na k**a jitihada za ziada zisipofanyika basi itabaki historia kuwa kulikuwa na Samaki wakubwa duniani.

26/07/2018

Mafia ni fungu visiwa la Tanzania pamoja na jina la
kisiwa kikubwa ndani yake inayotazama mwambao wa
Afrika ya Mashariki km 130 kusini kwa Dar es Salaam
karibu na mdomo wa Mto Rufiji.
Umbali wake na bara ni km 16.
Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa km 49 na upana wa
km 16; eneo lake ni takriban km² 400. Inajulikana pia
kwa jina "Chole mjini" kutokana na mji wa kale wa
Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini
karibu na kisiwa kikuu.kisiwa hiki kimezungukwa na visiwa ngine vidogo vidogo ambapo vipo vinavyokaliwa na watu na vile ambavyo vimekuwa nikambi tu za wavuvi. Miongoni mwa visiwa vinavyokaliwa na watu ni Bwejuu, Jibondo, Juani na Chole.

Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 9 za mkoa wa Pwani
ikiwa na wakazi zaidi ya 50,000. Mji mkuu na makao
makuu ya wilaya ni Kilindoni .
Tarafa za wilaya ya Mafia zipo mbili ambazo ni kaskazini na kusini ikiwa na jumla ya kata 8 ambazo ni
Baleni
Jibondo
Kanga (Mafia)
Kilindoni
Kirongwe
Kiegeani
Mibulani
Bwejuu

Wakazi walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba
madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja na n**i, chokaa
na samaki. Kuna utalii inayosifiwa sana lakini idadi ya
wageni ni kidogo. Hasa Waitalia wamependa
kutembelea Mafia kwa sababu ya jina la kisiwa. Mafia
imemaanisha shirika la jinai la kuhofiwa lenye historia
ndefu katika Italia ya kusini hadi siku ya leo.
Historia
Kihistoria Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya
utamaduni wa Waswahili k**a vile miji ya Chole na
Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya
Sultani wa Omani baadaye ya Zanzibar .
Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia kutoka
Sultani ya Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya
Mashariki ya Kijerumani. 1915 Waingereza waliteka
kisiwa wakishambulia manowari ya Kijerumani ya SMS
Königsberg mdomoni wa mto Rufiji kutoka Mafia.ambapo inasadikika kuwa hadi hii leo masalia ya manowari hiyo bado ipo katika mto rufiji.
Baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika sio tena
Zanzibar.

Hii ni kilindoni_Mafia
21/07/2018

Hii ni kilindoni_Mafia

18/07/2018

ukirudi nyuma katika karne ya 8 kisiwa hiki kilifanya kazi kubwa ya kuunganisha kibiashara Asia Mashariki na Afrika Mashariki na Jina Mafia limetokana na neno la kiarabu "Morfiyeh" maana yake "kundi" or "archipelego" ambapo kwa kiswahili ni "mahali pa Afya"

kisiwa hiki kinawakazi zaidi ya elfu 50 wakati shughuli kuu ya kiuchumi ni Uvuvi, kilimo na Utarii.kuna vivutio vingi katika maeneo mbalimbali k**a vile Magofu ya Chole, Hotel za Utende, kuogolea na samaki wakubwa, kuzamia mji wa mawe wa jibondo,mnara mkongwe East Afrika wa kuongozea Meli na mengine mengi.

kisiwa kinaukubwa wa mita za mraba 394 na jumla ya kata 8 ambazo ni Baleni, Ndagoni, Kanga, Jibondo, Kilindoni, Kiegeani, Kirongwe na Mibulani. Mafia ni moja kati ya Halmashauri 9 zinazounda Mkoa wa Pwani.

Address

Box 85, Mafia
Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mafia Tourism Island posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share